loading...

Natumia mita ya remote/King’amuzi kuna mpangaji ameondoka au ameharibu king’amuzi, nifanye nini?

Jina halisi ni CIU na sio king’amuzi au remote,mteja anayeibiwa au kupoteza CIU anapaswa kutoa taarifa kituo cha polisi ili kupatiwa loss report (Taarifa ya kuonyesha kuibiwa) kisha ataaandika barua kwenda kwa meneja wa Mkoa husika huku akiambatanisha taarifa ya polisi (loss report) mara baada ya wataalamu wetu kujiridhisha  mteja ataruhusiwa kulipia kiasi cha  Tsh 70,800.00 kama ni cha njia moja (Single moja) au Tsh 236,000.00 kama ni cha njia tatu (Three phase).