

[18:28, 31/07/2023] Neema Mbuja: Waziri wa Nishati, January Makamba ameeeleza namna alivyompata Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande akisema alimfanyia usahili wa muda mfupi kabla ya kupendekeza jina lake kwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyemteua.
Septemba mwaka 2021 Rais Samia alimteua Chande akichukua nafasi ya Dk Tito Mwinuka.Kabla ya uteuzi alikuwa mkurugenzi mtendaji wa kanda ya Afrika mashariki na magharibi wa Multichoice Afrika.
Waziri Makamba amefichua siri hiyo leo Jumatatu Julai 31, 2023 katika kongamano la Mwananchi Jukwaa la Fikra (MTLF), kwa ushirikiano na Tanesco, shughuli iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka 10 na safari ya mabadiliko ya kualiangaza Taifa.
Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga me…
[18:28, 31/07/2023] Neema Mbuja: Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu amesema mabadiliko ya katika taasisi za umma hayaepupikiki ilia kuleta ufanisi, akisema Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco), limeonyesha mfano katika mchakato huo.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan anataka mageuzi ya kila taasisi za umma, akisema Ofisi ya Msajili ya Hazina watakuwa wakiangalia uongozi na nafasi ya za bodi katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Pia watakuwa wakiangalia nafasi za bodi na menejimenti katika kufanya uamuzi kwa mujibu wa taratibu zao sambamba na kuwawezesha katika mitaji," amesema Mchechu.
" Tunategemea matokeo ya taasisi ni kutengeneza faida zitakazozalishwa na kuingizwa Serikalini au kujiendesha pasipo utegemezi wa Serikali kuu," amesema Mchechu aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 13, 2023 katika kongamano la Mwananchi Jukwaa la Fikra (MTLF), kwa ushirikiano na Tanesco, mchakato uliokwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa safari ya mabadiliko ya kuliangaza Taifa na ripoti ya mpango mkakati wa miaka 10 ya shirika hilo.
Mchechu amesema wamakubaliana kila taasisi za umma kutekeleza majukumu yao kwa uwazi ikiwemo kuwasilisha taarifa zao kwa wakati kuhusu utendaji wao ili kuwafanya wananchi kujua.
Katika hatua nyingine, Mchechu amesema bodi ya Tanesco itarudishiwa mamlaka yote ya kuendesha shirika hilo ikiwemo kuajiri sambamba na maslahi yao.Akisema Ofisi ya Msajili wa Hazina itakuwa ikiangalia vigezo vya utendaji kazi ili uhuru wao uendane na uwajibikaji.
" Hili litafanyika pia katika taasisi zenye mikakati mizuri kama ambavyo Tanesco ilivyo, lakini tutakwenda katika taasisi zote ili kuzipa uhuru.Tunatarajia kwa taasisi zingine viwango vilivyofanywa na Tanesco basi ndivyo vikubalike," amesema Mchechu.