Nataka kufunga mita ya pili kwenye nyumba yangu ili nijitenganishe na wapangaji, nifanye nini?

Hakikisha mita ya kwanza haina deni au haikuchezewa. Fika ofisi za TANESCO na kitambulisho utapatiwa fomu hakikisha unakuja na namba ya mita ya mwanzo. Baada ya hapo hatua zote ambazo mteja amezipitia kuomba umeme awali zitafuatwa kama ambavyo tumeonyesha kwenye sehemu ya taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme.