HATUA YA KWANZA* *(MAOMBI YA MWANZO

?Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika ndani ya kanda yake bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

?Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

?Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

?Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa na umekamilika (orodha zao zipo TANESCO)

?Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, Kitambulisho cha taifa nk (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

?Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa maandishi wa ruhusa ya mwenyenyumba. mteja anashauriwa kuja na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni. *(kama mita ya awali ina deni hatoruhusiwa kuomba mita ya pili)*

?Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya husika.

?Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika au la taasisi husika

?Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

?Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo:-

?Kuisoma fomu ( Mkataba wa kufungiwa umeme baina ya mteja na TANESCO) kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja hadi kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

?Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za TANESCO. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

?Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

?Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

?Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana hapo chini:

*Muda wa kupimiwa ka kupewa makadirio*

?Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu) *Ndani ya siku 7 za kazi*

?Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100) *Ndani ya siku 10 za kazi*

?Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)
*Ndani ya siku 14 za kazi*

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya TANESCOA ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (Control Number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms).wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena TANESCO bali TANESCO watakuwa na taarifa zake zote kupitia mifumo kuwasiliana na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

?Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu) *mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 30 za kazi*

?Kama ujenzi wa njia ya nyongeza utahitajika (mita 30- 100) *mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 60 za kazi*

?Kama mfumo mpya wa usambazaji utahitajika kujengwa au mfumo wa umeme mkubwa utahitajika kujengwa ( kama hakuna mfumo eneo husika) yaani zaidi ya mita 100 kutoka kwenye nguzo ya TANESCO *mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 90 za kazi*

KWA MAULIZO WASILIANA HUDUMA KWA WATEJA

?Kituo cha huduma kwa wateja Makao Makuu: - 0768985100/0222194400

?Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

?Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

?Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

?Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
?WhatsApp za huduma kwa wateja Nchi nzima

 *ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA ZETU*

 *TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO*