Waziri Makamba SCADA SEPTEMBA1Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba wakati akikagua kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme wa Gridi ya Taifa, leo Septemba 17,  2021 amesema atahakikisha TANESCO inakuwa Shirika bora Afrika Mashariki.
 
Aidha amewataka watendaji wa Shirika kujianda kwa mabadiliko makubwa yenye tija yatakayo saidia kuimarisha Shirika ili kuongeza tija na ufanisi.
 
Mhe. Makamba ameagiza TANESCO kuhakikisha wanatatua matatizo ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini, ambapo ametoa wiki mbili kwa wataalamu kuhakikisha wanatatua tatizo hilo kwenye maeneo mbalimbali.
 
Lengo la Mhe. Makamba kufika kwenye kituo cha kudhibiti mifumo ya umeme wa Grid ya Taifa kilichopo ubungo Dar es salaam, ni kujifunza na kuelewa kuhusu mfumo  mzima  wa Grid ya Taifa.
 

Mhe. Makamba amesema Shirika lina mambo mengi ya kufanya kama uwekezaji mbalimbali na kuongeza wateja Nchi nzima ili kuweza kufikia adhima yake yakua shirika bora Afrika Mashariki.