loading...

.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande  amesema safari ya mabadiliko ndani ya shirika hilo ilianza kwa kujipanga ikiwemo kwenda kila mkoa ili kujua changamoto za wananchi.

Chande amesema hayo leo Jumatatu Julai 31, 2023 katika kongamano la Mwananchi Jukwaa la Fikra (MTLF) kwa ushirikiano na Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco).Kongamano lilikwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa safari ya mabadiliko ya kuliangaza Taifa na ripoti ya mpango mkakati wa miaka 10 ya Tanesco.

" Kujipanga ni kwenda kila wilaya, mkoa  na kitongoji kujua matatizo ya wananchi na kuanisha mipango ya kuyatatua. Sasa hivi tunafahamu matatizo yote na majawabu yake.

"Kazi hii tulianza na kuimaliza sasa hivi tupo awamu ya pili ya kutekeleza yale yaliobainika, tunaamini 2026/27 tutakuwa tupo vizuri kwa sababu matatizo mengi yatakuwa yamekwisha na tutakwenda vizuri," amesema Chande.

Mbali na hilo, Chande amesema faida ya Tanesco imeongezeka kutoka Sh77bilioni kwenda 109.4 bilioni. Hata hivyo, amesema faida hizo zitaelekezwa zaidi katika biashara ili kuboresha huduma za shirika.

 

"Tanesco imeweza kupunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 15 iliyokuwapo hadi kufikia asilimia 14.5," amesema Chande.