”TANESCO MNAFANYA KAZI NZURI “ Mhe.Biteko
Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko amelipongeza shirika la Umeme Nchini ,TANESCO kwa kuendelea kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha Wananchi wanapata nishati ya umeme.
Mhe. Biteko ameyasema hayo Aprili 16,2024 wakati akifungua maonesho ya wiki ya Nishati katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
“TANESCO nawapongeza sana siku hii ya maonesho, mnafanya kazi kubwa endeleeni na moyo huo, akitokea mtu anawarudisha nyuma, kwa utaratibu wenu wa ndani mwambieni usiturudishe nyuma” amesema Mhe. Biteko.
Mhe.Biteko pia ameeleza namna ambavyo TANESCO imeendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kutoa huduma kwa wananchi.
“Wakati huu wa mvua nyingi, zilizosababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali Nchini,Nguzo nyingi sana zinaanguka, TANESCO wanafanya kazi kubwa sana kurudisha miundombinu ya umeme kuwa katika hali ya kawaida, Kuna mahali ambapo hata njia ya kufikisha nguzo haipo lakini wanapeba nguzo zile hata kwa matoroli ya punda ili watu waweze kupata umeme” amesema Mhe. Biteko
Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu amempongeza Naibu Waziri mkuu na Waziri wa nishati, Mhe .Biteko kwa kuthibiti changamoto za upatikanaji wa umeme nchini.
“Kwa sasa umeme tunauona kwa ukamilifu mkubwa sana,Magrupu ya wateja ya kulalamikia umeme sasa hivi mengi hayana wachangiaji kwa sababu umeme upo tofauti na mwaka uliopita,sasa hatuoni malalamiko yale” amesema Mhe. Zungu
“Mimi ni moja kati ya wabunge niliokuwa nikikusumbua sumbua sana katika maswala ya nishati. Natamka kwamba kuanzia leo sikusumbui tena kwa sababu nimejionea mimi mwenyewe, nina macho ninaona na nina masikio nasikia kwamba Tanzania tuliyokuwa nayo miaka mitatu iliyopita sio Tanzania ya sasa hivi katika masuala ya nishati”
Nae mbunge wa Kinondoni Mhe. Abass Tarimba amesema awali alikuwa anapata changamoto kubwa katika suala la umeme kwa wananchi wake lakini kwa sasa hali imebadilika.
“Mimi ni moja kati ya wabunge niliokuwa nikikusumbua sumbua sana katika maswala ya nishati. Natamka kwamba kuanzia leo sikusumbui tena kwa sababu nimejionea mimi mwenyewe, nina macho ninaona na nina masikio nasikia kwamba Tanzania tuliyokuwa nayo miaka mitatu iliyopita sio Tanzania ya sasa hivi katika masuala ya nishati” amesema Mhe. Tarimba
Maonesho ya wiki ya nishati yanaendelea katika viwanja vya Bungr jijini Dodoma na yatamalizika Aprili 19, 2024 ambapo Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati zimeshiriki katika maonesho hayo, Lengo kuu likiwa ni kuleta mrejesho kwa wabunge juu ya mwaswala mbalimbali yanayohusu wizara ya Nishati ikiwemo majibu ya changamoto za Umeme katika majimbo yao na mrejesho wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali .