MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA MATUKIO YA MOTO UNAOSABABISHWA NA UMEME MAJUMBANI.
- Hakikisha utandazaji nyaya (wiring) inafanywa na mkandarasi aliyesajiliwa na Serikali
- Hakikisha vifaa vyote vinavyofungwa vimethinitishwa na TBS (K.m: nyaya, soketi swichi, saketi breka na main swichi)
- Hakikisha waya wa ethi umethibitishwa na TBS na umechimbiwa chini ardhini inavyotakiwa
- Hakikisha unapotumia pasi usiiache ikiwaka ukaenda kufanya kazi nyingine. Vyivyo hivyo tutumiapo hita za kuchemshia maji na majiko ya umeme.
- Tusinyooshe nguo kwa pasi ya umeme kitandani
- Tuepuke utumiaji wa extension cable wa kudumu. Zitumike kwa dharura tu. Pia tusiweke extension cables kwenye mazuria (carpets)
- Tusichaji simu na kuziweka kitandani. Pia tusitumie kompyuta mpakato (laptops) tukiwa tumezieka kitandani
- Tusi plagi vitu vingi vinavyotumia umeme kwenye soketi moja kwa mfano TV radio na friji kwenye soketi moja
- Tusiweke mapazia marefu kwenye madirisha yanayofunika soketi za umeme
- Tutumie mapazia yasiyoshika moto kwa urahisi; kwa mfano mapazia ya nguo za pamba
- Tuangalie magodoro ya vitanda yasikaribie au kugusa sokti au swichi za umeme
- Makochi yetu tusiyaweke yakagusa au kukaribia sana swichi au soketi ya umeme. Yawekwe angalau umbali wa inchi sita (15sm)
- Vyandarua vya vitanda visisogelee swichi au soketi ya umeme
- Tupunguze wingi wa vitu vinavyoweza kuwaka moto ndani ya nyumba; kwa mfano, ni vizuri kuwa na seti moja tu ya makochi
- Kama umeme ulikuwa umezima, ukiwaka tena kitu cha kwanza tuhakikishe mishumaa yote tuliyoiwasha wakati umeme umezimika tumeizima.
- Kama fyuzi ya umeme itakatika au soketi breka ikajizima, tuhakikishe tumemwita fundi kukagua kwa nini ilizima. Tusiweke fyuzi nyingine au kuwasha tu saketi breka.
- Tuhakikishe tunamwita mkandarasi aliyesajiliwa kupitia mfumo wote wa umeme kwenye nyumba (hasa maungio yote) kila baada ya miaka mitano
- Tusiongeze vitu vinavyotumia umeme mwingi kama viyoyozi bila kuwahusisha makandarasi waliosajiliwa kuangalia uwezo wa mifumo yetu ya umeme kuhimili mzingo unaoongezeka.
- Tusiunganishe umeme kutoka nyumba moja kwenda nyingine au kwenda kwenye banda la kuku bila ya kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa
- Ikitokea hitilafu yeyote ya umeme kuanzia kwenye mita ya TANESCO, braketi nguzo na kwenye laini ya umeme, tutoe taarifa katika kituo chochote cha TANESCO kwa kutumia namba za dharura.